USIPOTELEE NDANI YA WOKOVU
PRE; PASTOR OMERY DEO LESSON: SALVATION {WOKOVU} Mwanadamu ameumbwa ili aishi katika {Dunia} ardhi iliyofanywa na MUNGU mwenyewe, mwanadamu anapoishi duniani anaishi katika mazingira ambayo ni sahihi kabisa kama vile MUNGU alivyokusudia tangu alipomuumba na kumweka pale Eden. Lakini kwa sababu ya tabia ya uasi ya mwanadamu aliyoiruhusu yeye mwenyewe kwa kumsikiliza yule ASI, amejikuta anaishi katika mifumo mibaya ya maisha katika dunia sahihi, HAKUNA SABABU MWANADAMUN KUICHUKIA DUNIA. Amejikuta anajiona kuwa haishi mahali sahihi ingawa ni mahali sahihi iwake, kwa sababu tayari ameupoteza uhusiano mzuri kiati yake na mazingira anayoyaishi mwenyewe. ...