USIPOTELEE NDANI YA WOKOVU
PRE; PASTOR OMERY DEO
LESSON: SALVATION {WOKOVU}Mwanadamu ameumbwa ili aishi katika {Dunia} ardhi iliyofanywa na MUNGU mwenyewe,
mwanadamu anapoishi duniani anaishi katika mazingira ambayo ni sahihi kabisa kama vile MUNGU alivyokusudia tangu alipomuumba na kumweka pale Eden.
Lakini kwa sababu ya tabia ya uasi ya mwanadamu aliyoiruhusu yeye mwenyewe kwa kumsikiliza yule ASI, amejikuta anaishi katika mifumo mibaya ya maisha katika dunia sahihi,
HAKUNA SABABU MWANADAMUN KUICHUKIA DUNIA.
Amejikuta anajiona kuwa haishi mahali sahihi ingawa ni mahali sahihi iwake, kwa sababu tayari ameupoteza uhusiano mzuri kiati yake na mazingira anayoyaishi mwenyewe.
MWANZO 19:30-38
Mwanadamu anapoishi duniani hujikuta akichoka na kulemewa na masumbufu ya maisha anayoyaishi mwenyewe, amejikuta akiingia kwenye mfumo wa maisha ya utumwa, akijikuta KUMZOELEA MUNGU.
Kamwe Mungu hazoeleki.
Hapa tunamwona LUTU alipopanda kutoka SOARI, akakaa mlimani kwa sababu tu aliogopa kukaa Soari.
2 Samweli 6:1-7 Habari ya mtu mmoja aliyeitwa UZA, huyu ndugu nbalikuwa karibu sana na MUNGU, yaani alikuwa karibu sana na MAKUHANI.
Makuhani walikabhiwa SANDUKU LA AGANO walibebe mabegani, ilikuwa ni agizo la Mungu kwao kuwa ni lazima walitwae mabegani mwao, lakini baadaye wao wakaamua kuboresha namna ya kulibeba, wakatengeza gari lililokuwa likivutwa na wanyama {ng`ombe}, Mungu naye akakaa kimya.
KISA:
Ilikuwa yapata siku moja wakiwa wamelibeba katika gari hilo, hilo sanduku likaelekea kudondoka, ndipo Uza {hakuwa Kuhani}, akalizuia kwa mikono yake ili lisianguke chini, ghafula likamwangukia yeye na kumponda akafa.
Uza hakuwa na makosa, bali kosa lilikuwa juu ya Mkauhani waliotakiwa kulitwaa mabegani mwao wasifanye hivyo.
FUNZO:
Kilichowaponza wale Makuhani ni kule kumzoelea Mungu, yaani walimtumikia kwa mazoea, Mungu akakasirika, wakamponza UZA.
Lakini pia kingine kilichomponza Uza ni kuyagusa mafuta ya Makuhani, ile haikuwa kazi yake kuhangaika na lile SANDUKU LA AGANO.
KATIKA MAISHA YA WOKOVU HATUTAKIWI KUYAZOELEA na kuona wokovu kuwa kama kitu cha kawaida, Wokovu ni kama jengo lililojengwa nasi tukafichwa humo kwa tendo la MUNGU kutuhamisha kututoa katika Ufalme wa giza na kutuingiza katika UFALME WA NURU WA MWANA WA PENDO LAKE
Wakolosai 1:13.
MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA NA KUKULINDA.
Wakati haunitoshi nkukuletea habari ya mashujaa wa IMANI waliomshawishi MUNGU hata akawaita Rafiki zake
WABRANIA 11:1-................
Kiwango cha ukaribu wako na MUNGU utaendelea kuongezeka kwa kadri unavyozidi kujifunza NENO LA MUNGU KILA WAKATI,
Zaidi sana viwango vyako vya IMANI vikiongezeka na hata kumshawishi MUNGU AKAKUITA RAFIKI YAKE.
.................huu sio wakati wakuuzoelea WOKOVU huu tuliopewa kwa gharama kubwa sana.
Maoni
Chapisha Maoni