NGUVU YA HASIRA

SEHEMU YA PILI UCHAMBUZI
    Mwalimu: BABU  NA  BIBI                     

KITABU: WAKOLOSAI 3:8.................

                                  Bwana Yesu asifiwe Mtumishi wa Bwana,
 unayesoma ujumbe huun na unayeendelea kufuatana nasi katika mfululizo wa masomo yetu yanayoendelea hapa jijini Dar Es Salaam, 
katika kanisa la PENTECOST TEBARNACLE OF PRAISE,
 TEGETA KIBAONI.

Sasa tuendelee....................
                                      Katika kitabu hiki cha wakolosai sura ya 3 inatupa nuru na mwanga wa kutosha kabisa kuweza kung`amua mambo mengi sana 
yatupasayo kuyaendea zaidi sana kumjua MUNGU.  

                        Mstari wa 8 na kuendelea tunakutana na ujumbe mzito sana kuhusiana na                       HASIRA.
Tunasoma;
 8.  Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu wote, na matukano, na matusi vinywani mwenu. 
    
           Biblia inaongea vitu vizito mno ambavyo ukivitazama na kuvichunguza utabakia umeduwaa tu na kuchanganyikiwa ukiwa nje ya usaidizi wa Roho Mtakatifu.

Biblia inasema tuwe na hasira lakini tusitende dhambi,
 kwa maana nyingine kuwa na hasira sio dhambi,
 bali unapoitumia hiyo hasira vibaya katika maamuzi ndipo unapoweza kutenda dhambi.

        Unashauriwa ukiwa na akili timamu usifanye maamuzi ya aina yoyote ile ukiwa katika hali ya hasira, 
Maandiko yako wazi kabisa ya kwamba
 "Hasira ya mwanadamu siku zote haitendi haki ya Mungu." 

Hata MUNGU hayuko tayari kukuruhusu usogee mbele zake ukiwa na hasira, maana hutaelewana naye pindi utapokuwa unaingia kuabudu.

                      HASIRA NI MBAYA NA NI NZURI PIA 
            Inakuwa nzuri pale unapooneshwa namna ambavyo hukufurahishwa na tukio au tendo fulani lililotendeka kinyume na matarajio stahiki.
                 unaonesha hasira kumfanya mtuhumiwa au mkosaji kujitambua na kugundua ya kwamba alichokifanya si sawa.
Pindi atakaporekebisha na kubadilisha mwelekeo ndipo utakapoiona faida ya hasira na uzuri wake, 
                      lakini unashauriwa usifanye maamuzi ya aina yoyote yale dhidi ya kile au lile ambalo hukufurahishwa nalo .  USIAMUE PEKE YAKO BALI WAENDEE WALI JIRANI NA WEWE WAKUINUE ikiwezekana.

                        FAIDA YA HASIRA ni kuyakemea yale yasiyofaa,
 ushahidi juu ya hili tunauona kwa Bwana Yesu  alipowakuta watu wakifanya biashara katika nyumba ya Mungu,
 aliwakemea kwa hasira na kupindua pindua meza na viti vyote na kila kilichokuwemo ndani yake. 


                                 Kolosai 3;12
               Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo rehema, utu wema, un yenyekevu, upole, uvumilivu, 
 13. mkichukuliana na kusameheana.

Zaidi ya yote ni kukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu na Mungu pia.


MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA NA KUKULINDA ZAIDI YA YOTE 
USIWE NA HASIRA HATA IKAKUZALIA MATUNDA.

Kwa maana hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu ....................................................


                     Itaendeleaaaaaaaaa..........................   

                         MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI MSOMAJI WANGU NA                                        UZIDI KUFUATANA NASI KTK MWENDELEZO WA MASOMO HAYA.

                                Ni mimi ndugu yako na rafiki yako 
                                     Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
                                          elimelck@gmail.com  

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

JE, UNAIJUA KARAMA YAKO? By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe