KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

Na Pastor Omery Deo Shinze

Mwanadamu ana mfumo wa pekee wa maisha au namna ya kuishi tofauti na viumbe wengine wote.

       Kila iitwapo leo, mwanadamu anayeishi anatamani kuwa na mabadiliko chanya, yaani maendeleo.

Tunaporejea kiroho sasa, mwanadamu anahitaji kuchukua hatua ya juu zaidi kuendelea kiroho.

VIWANGO VYA KUMJUA MUNGU vinatakiwa kuongezeka kila iitwapo Leo.

Hautakiwi kuridhika na hatua uliyonayo au kiwango ulichomo,

Mfano, kama ulikuwa ni muimbaji, usiishie tu KUIMBA bali baada ya hapo utoke sasa ukatabiri, ukahubiri, ukafungua vituo vya umishonari (kanisa) umtumikie mum kwa viwango vingine vya juu zaidi.
MATHAYO 28:19 Hili ni agizo kuu la Kristo kwa kanisa.

Mfano,
mwanajeshi hadi mwanajeshi kamili huwa anaanzia hatua ndogo ndogo ndiposa baadaye huongeza mazoezi yaliyo bora au magumu zaidi ya yale ya mwanzo.

Haijalishi umeomba dakika ngapi na MUNGU hajakujibu, wewe ongeza masaa, siku, wiki, miezi .........usikate tamaa.

MARKO 2:1-5
Mtu Mmoja nchini Capernaum, alikuwa mgonjwa hajiwezi,

Baada ya kusikia habari za Yesu Kristo, na hata alipokaribia hakuweza kumuona YESU maana mkutano ulikuwa umesonga,
          4. Wakaamua kutoboa dari ili Waweze kumfikia Yesu.

NB: UKIONA UMETUMIA NJIA FULANI IKASHINDIKANA, BASI TOBOA DARI, AU TUMIA NJIA MBADALA.

DON'T GIVE UP, usikate tamaa.

Kukata tamaa ni kukubali kushindwa na kumpa adui nafasi ya kutembea na mafanikio yako.

Haijalishi umesongwa kiasi gani, wewe TOBOA DARI, yaani tumia njia nyingine zaidi.

Usikubali adui atoboe Dari la nyumba yako, Bali wewe TOBOA kwake.

1 WAFALME 3:16-27
Wanawake wawili waliokuwa makahaba, walimwendea mfalme Sulemani, wakigomea mtoto..........

     (Madhara ya kulala usingizi usio na faida).

........kwa uamuzi alioutoa Sulemani, haikuwa hekima ya kawaida, hadi maadui walimuogopa
1 Wafalme 4:21, 29, 30, na 34. Wamisri wakletea tunu na kumtumikia siku zote za maisha yake.

Ng'ang'ania baraka za Bwana, usiondoke bila kuzipata.

LUKA 19:1-8 Yesu akafika Yeriko, akamkuta jamaa Mmoja aitwaye Zakayo, ................ ............akakwea juu ya mkuyu.

Zakayo ktk jamii yake alionekana kuwa mdhurumaki na MTU mbaya kabisa.

Lkn ktk SAA asiyoidhani, WOKOVU ukafika nyumbani mwakeye.

Kanuni ya Yesu Kristo hapiti uchochoroni, Bali NJIA KUU (High Way).

Zingojee baraka zako ukiwa mahali sahihi.

NB: NI AHERI MBILIKIMO (UFUPI) WA MWILI
KULIKO MBILIKIMO WA KIROHO.

Wafupi wa kiroho huwa ni wasumbufu mno kanisani, huwa hawaelewi chochote,

MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

NGUVU YA HASIRA