BIBLE STUDY 4th DAY
MH; BABU & BIBI
SOMO: UCHAMBUZ WAKOLOSAI SURA YA NNE {KOL 4:1-18}

LEO TUNAENDELEA NA SURA YA NNE YA KITABU CHA WAKOLOSAI
MST 1-2 "Ninyi akina bwana wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili,
mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana Mbinguni.
2. Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukurani.
Mtume Paulo alikuwa akiongea na watu wale ambao wanaishi na watumishi majumbani mwao {wafanya kazi}, akichukulia mfano wa utumishi katika nyumba ya Bwana, Akiwakumbusha namna wanavyoweza kuishi nao kwa uzuri sawa na vile wao walivyo chini ya Bwana mwingine ambaye ni Mungu wa Mbinguni.
Lakini pia akiwakumbusha kuwapongeza pale wanapokuwa wametenda vema na kuwafundisha yaliyo ya adili, yaani wajiheshimu na kuepukana na kila namna ya ubaya.
Mstari wa tatu,
anawakumbusha juu ya kuomba na zaidi sana wakidumu katika kuomba na kuwaombea wengine,
lkn pia akiwasihi kuwa na tabia ya shukrani kwa Mungu wa Mbinguni.
Mfano
Kwa watumishi wa Mungu, wameagizwa kuwa na HEKIMA popote waendako hasa mbele yao wasio na hekima.
Mfano unapohubiri katika makusanyiko ya watu billa taarifa, usiwadai sadaka.
Au ukiwa unahubiri ndani ya daladala pia usiwaombe sadaka pale unapokuwa umemaliza kuhubiri.
HEKIMA
Tunapoitamka hekima moja kwa moja tunakuwa tunamtaja YESU KRISTO mwenyewe maana yeye ndiye hekima yetu.
WAKOLOSAI 4:5-6 "Enendeni kwa mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.
6. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Biblia iko wazi kabisa, inatufundisha kutembea na Yesu ndani yetu na tukifanya kazi pamoja naye pia. Unapotembea na Yesu utajikuta yeye pia anakuelekeza namna ya kutembea na kuwafikia watu wa aina mbalimbali na tofauti tofauti pia.
Lakini pia atakufundisha namna ya kuongea nao na kuwajibu pindi waulizapo juu ya tumaini lako [WOKOVU].
Tuwe tayari wakati wote kuwajibu watu watuulizao habari ya tumaini letu, lakini kwa hekima tuyakimbie maswali yawezayo kuleta fujo na magomvi.
KUNA UTOFAUTI ULIOPO KATI YA kufanya kazi ya MUNGU na kufanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU,
Unapoifanya kazi ya Mungu,
bila kuifanya na Mungu mwenyewe utajikuta unatembea peke yako bila kuwa na msaada wa kiMungu,
mahali hapa ndio wengi wamejikuta wanafanya huduma,
wanachoka nakuishia njiani.
Kufanya kazi bila kuifanya pamoja na Mungu utajikuta unaifanya ukiwa mkavu bila hata kuitumia nguvu ya MUN GU,
Kazi ya Mungu bila Mungu inaweza kufanywa na mtu yeyote
hata mpagani anaweza akaifanya pia na akajiona yuko sawa kabisa. Bila kujali ameokoka au laa.
UTOFAUTI UNAKUJA pale unapoifanya huduma au kazi ya Mungu ukiwa pamoja na Mungu mwenyewe, hapa ndipo sasa tunasema kufanya huduma kwa HEKIMA, maana yake uifanye kazi pamoja na Yesu MWENYEWE.
Zaidi ya yote, mtumishi wa Bwana bila kujidharau na kukata tamaa, tafuta kwa bidii kuifanya kazi ya Mungu pamoja na Mungu mwenyewe.
Usiiache hekima ikawa mbali nawe.
MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI NA KUKUVUSHA NG`AMBO YA MAISHA YAKO KIROHO NA KIMWILI PIA.
LINAENDELEAAAAA.............................
KARIIIIIBU KANISA LA PENTEKOSTE HEMA YA SIFA, TEGETA KIBAONI.
Imeletwa kwako nami Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
Email; elimelck@gmail.com
+255715445846
+255684485460
Powerfully and blessing messege
JibuFuta