BIBLE STUDY

MH; BABU  &  BIBI
SOMO;  SURA YA PILI YA KITABU CHA WAKOLOSAI

                                 Mtumishi wa Mungu PAULO aliiandika hii sura kwa ajili ya watu wa MUNGU, ambao tayari wamekuwa wafuasi wa Mungu kwelikweli kwa njia ya YESU KRISTO.

                       Amejaribu kulikumbusha kanisa kwa habari ya kujitambua na kujua wito wao mkuu,
akiwasihi kuishi wakiifuata njia ile iwapasayo kuiendea ambayo walihubiriwa kwa hapo mkwanza na Yesu mwenyewe, 

                         Zaidi sana akiwasihi kuyatafakari yale yaliyo juu zaidi kule Yesu aliko  {mstari 1},
anasema, Basi ikiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.

UHAI 
                        Hili ne neno zaidi ambalo tunakutana nalo katika sura hii ktk 
Kolosai 3:3-4 "Kwa maana mlikufa , na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo nanyi mtafunuliwa katika utukufu."

                                          Mtume Paulo anatuonesha namna ambavyo inatupasa kuishi sisi kama watoto wapendwao wa Mungu Baba yetu wa Mbinguni.

                    Kolosai 3:5 "Basi vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu tamaaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;  
6. Kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.

                    HAPA TUNAKUTANA NA MAMBO KADHA WA KADHA
1. UASHERATI
                   Haya ni mahusiano ya tendo la ndoa ambayo hufanywa na watu ambao bado hawajaingia kwenye ndoa, yaani bado hawajaoa wala kuolewa. 
Huu ni uchafu kama uchafu mwingine tu ule unaoufahamu wewe msomaji wangu.

2. UZINZI
                  Haya nayo ni mahusiano pia ya tendo la ndoa ambayo huwahusisha wanandoa ambao huamua kuziacha ndoa zao na kwenda nje ya ndoa zao, Tendo hilo huitwa uzinzi.    

Mungu alianza na Wayahudi kuwapati mifumo namna ya kuishi na ndoa zao, yaani aliwapatia utaratibu mzuri namna wanavyoitakiwa kuishi katika ndoa.

3. TAMAA MBAYA
              Kuwa na tamaa sio dhambi, but inakuwa dhambi pale unapoigeuza hiyo tamaa uliyonayo katika hali ya ubaya. Maana yake unakuwa na tamaa mbaya yenye nia mbaya kwa ajili yako nmwenyewe na jirani yako.                 Mtume Paulo ametukataza kuwa na tamaa mbaya kuwa Mungu huchukizwa nayo. 

         NB: Ndanmi ya Tamaa mbaya utakutana na mawazo mabaya, shauku mbaya, ambayo haya yametajwa kuwa ibada ya sanamu 

Mawazo mabaya husababisha mwanadamu kuleta vita au kutamani madaraka pamoja na kutamani mwanamke  mwingine au mume wa mtu.

Lakini pia nchi nyingi duniani zimeingia katika migogoro mikubwa kwa sababu ya matokeo ya tamaa mbaya baina ya watawala au koo na jamii mbalimbali.

CHOCHOTE KILE UTAKACHOKIPENDA KULIKO MUNGU  UJUE HIYO NI SANAMU KWAKO.

NI lazima Mungu awe wa kwanza katika maisha yako na yangu pia.

                                ASANTE SANA MSOMAJI WANGU NA MTUMISHI WA MUNGU PIA, 
                                MUNGU ANAKUPENDA KULIKO UNAVYODHANIA.

SOMO hili limefundishwa na watumishi wa Mungu  BABU NA BIBI

Na kuletwa kwako nami Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
                                          Email: elimelck@gmail.co

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

JE, UNAIJUA KARAMA YAKO? By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe