USIMUOGOPE MFALME WA ASHURU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu . Karibu tujifunze Neno la MUNGU. MUNGU akupe Neema juu ya ujumbe huu, ukaone Neema ya kutokea Ukaone nguvu ya MUNGU ikiambatana na wewe kupitia Neno lake. Kumbuka Biblia inasema katika Zaburi 107:20 kwamba " Hulituma neno lake, huwaponya , Huwatoa katika maangamizo yao ." Kwa hiyo Neno la MUNGU ambalo MUNGU huwa analiachilia, analituma lije kwako wakati mwingine lina kazi nyingi. Kazi mojawapo ya Neno hilo ni kuponya, kazi mojawapo ni kukuondoa kwenye maangamizo , kazi nyingine ni kukuimalisha , lina kazi nyingi Neno la MUNGU , ni zaidi ya kazi kumi Neno la MUNGU linaweza likafanya katika maisha yako . Ujumbe wa Leo ni Neno limetumwa kwako ili kukuambia kwamba usimwogope Mfalme wa Ashuru . ...