BIBLE STUDY 6Th DAY
SEMINA YA WANACHUO CHA BIBLIA
MH: BABU NA BIBI
SOMO: WAGALATIA SURA YA NNE
{URITHI, UHURU NA UTUMWA}
Bwana Yesu asifiwe ndugu yangu mpendwa, natumai ya kuwa u mzima wa afya tele na Neema ya Mungu inatembea upande wako.
Ni wakati mwingine tena nikufikishie ujumbe huu ambao tunaendelea nao hapa kanisani tukiwa na walimu wetu hawa {BABU NA BIBI}.
Leo tulijifunza kitabu cha Wagalatia sura ya Nne. Kuna mambo mengi sana tumeyaona hapa na kujaribu kujifunza na kukumbushwa mambo kadhaa juu ya safari yetu hii tuliyonayo ya kwenda Mbinguni.
WAGALATIA 4;1........ Lakini nasema ya kuwa mrithi wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote.
2. bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba`
Mtume Paulo ameongea vitu vya ajabu sana hapa,
amezungumzia kwa habari ya heshima ya URITHI, anasema nguvu ya mrithi inaonekana tu pale ambapo atakuwa ni mkubwa,
bali awapo mtoto hawezi kukabhidhiwa maana hatakuwa na uwezo wa kumiliki na kutawala, nafasi yake itasalia pale pale ikilindwa na waaminifu hata atakapokuwa mkubwa.
KANISA LA WAGALATIA linakumbushwa kwa habari ya wokovu ambao uliwekwa akiba kwao na hata wakati ulipowadia akaja kwa ajili yao akawakabidhi wokovu.
GALATIA 4;3 Kadharika na sisis, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.
4. Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma mwanaye ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5. kusudi awakomboe wao walio chini ya sheria.....................................
lakini wamejikuta wanauzoelea na kuuona kama kitu cha kawaida sana kwao.
GALATIA 4:7-13
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Kadharika,
hapa tunakutana na maneno yanayozungumzia kuhusu mtume Paulo,
Anasema alikuwa dhaifu, anazungumzia udhaifu wa mwili, kwa maana nyingine alikuwa mgonjwa hatuwezi kusema alikuwa anaumwa na nini, ila kama mwanadamu tunaamini kuwa alikuwa anaumwa tu.
NI MUHIMU SANA kujua na kuijali afya ya miili yetu ili iwe na afya njema.
2 WAKORINTHO 11:22-27 Paulo kama mwanadamu katika utumishi wake alipitia mapito mengi sana na majaribu mengine ya kukatisha tamaa,
Waumini wakiyafuatilia mafundisho kwa umakini zaidi katika ibada
iliyokuwa ya Baraka tele
KITABU cha Wakorintho kiliandikwa miaka kumi na tano baada ya kuandikwa kitabu cha Wagalatia.
Pamoja na mazingira magumu aliyopitia Paulo, lakini bado hakukata tamaa wa kufia njiani wala kupunguka kiimani.
GALATIA 4:17-20 Alikuwa akiongea na Mafarisayo na wale wazee na Walimu wa Sheria ambao waliishi TORATI na kutaka kuyaendeleza mapokeo ambayo yalikuwa manyonge.
Paulo aliuonesha utungu aliokuwa nao kwa ajili ya Wagalatia ambao wakati mwingi walijikuta wakijisahau na kuyarejea tena mafundisho manyonge {ANDIKO}, Mafundisho yaliyowalazimisha watu kuishika TOHARA YA MWILINI.
GALATIA 4:21-27 ukiifananisha na MWANZO 16:17-21
Habari ya Ibrahimu na mkewe SARAI.
Tunakutana na habari ya maisha yake namna ambavyo hata mke wake alipitia kipindi kigumu sana cha kukaa muda mrefu bila kupata mtoto, anapata utungu, anaugulia jinsi ambavyo alikosa furaha katika ndoa yakle.
Sara alifedheheka sana hata akafikia hatua ya kuwaza mabaya, pengine alihisi labda mume wake ana tatizo, au labda yeye mwenyewe ana tatizo kwenye uzazi,
Ikafikia hatua kama anajaribu aone wapi kuna tatizo, akamshawishi mumewe alale na mfanya kazi wake pengine atapata mtoto.
Na ikawa kweli, IBRAHIMU akaingia kwa mjakazi wake akalala kwake naye akapata mimba akazaa mtoto mwanamume, aliyepewa jina lake ISHMAELI.
ISHMAELI akazaliwa kwa mjakazi {HAJIRI], akalelewa pale, na ikawa Hajiri anamdhihaki SARAI, ndipo hasira ikawaka ndani ya Sarai juu ya mjakazi wake.
Ikapita miaka kumi na mitano baadaye akazaliwa mtoto kwa kwa SARAI,
katika uzee wake akampata mtoto ISAKA.
MWANZO 16:11-12 Hapa tunakutrana na habari ya Malaika anavyoteta na SARA.
NB: Katika uzao wa IBRAHIMU
IBRAHIMU anawakilisha taifa la Mungu linaloshambuliwa na maadui, lakini hatimaye anashinda.
SARA anawakilisha Kufunguliwa katikam vifungo m nbalimbali
ISAKA anawakilisha Uhuru au Uungwana
ISHMAELI anawakilisha Sheria ao Torati.
MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI MSOMAJI WANGU.
elimelck@gmail.com
Ni mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.
Niliyekufikishia ujumbe huu uliofundishwa na walimu wetu hapa hapa kanisani
HEMA YA SIFA TEGETA
Maoni
Chapisha Maoni