BIBLE STUDY

MHU: BABU  AND  BIBI
SOMO: MUHTASARI AU MAREJEO KITABU CHA WAGALATIA

Bwana Yesu basifiwe ndugu yangu Mpendwa,

                Baada ya kuwa tumefikia mwisho wa kujifunza kitabu hiki cha Wagalatia sura zake zote sita, walimu wetu waliweza kujiridhishakama wanafunzi tumefaidika na tumeelewa ninikatika KITABU HIKI CHA wagalatia.
Ongeza kichwa

MASWALI YA CHANGAMOTO
1. Nini hasa kilichokugusa katika kitabu hiki cha Wagalatia?
2. Kitabu cha Wagalatia kimewezaje kuyabadilisha maisha yako?
3. Utafanya nini ili usababishe mabadiliko katika maisha yako?

                       Kila mmoja wetu mwanafunzi darasani aliweza kutafakari ni namna gani alivyoweza kukielewa kitabu hiki cha WAGALATIA chenye sura sita tu.
     Ni kweli,
 kuna mambo mengi sana ambayo yameainishwa katika kitabu hiki, unaweza kuyaelezea na usiweze kuyamaliza kwa kadri Roho wa Mungu atavyokuwa akizidi kukufunulia na kukuionesha.

Mfano, 
WAGALATIA 1:6 "Nastaajabu sana kwa sababu mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika NEEMA ya Kristo, na kuigeukia Injili nya namna nyingine."

                              Hapa tunaona mtume Paulo anawaonya kanisa la Wagalatia akiwa kama mkombozi wa njia zao za ubatili, ambapo waliigeukia injili nyingine isiyo ya Kristo.
Na kanisa la leo linashauriwa kadharika kujifunza kuyachunguza maandiko na kuyafuata ka uzuri, usahihi na utakatifu.

============>Yako mengi sana ambayo yamewagusa wanafunzi darasani wote walioweza kufuatana na waalimu wetu waliokuwa nwakifundisha kitabu hiki cha WAGALATIA.

        Kitabu hiki kimeweza kuyabadilisha maisha ya wengi, na hata sasa bado kinazidi kuyabadilisha maisha ya wengi kwa kiwango kikubwa sana endapo tu utakuwa tayari kujifunza Neno la Mungu na kuikataa injili ya namna nyingine isiyo ya Kreisto.

               Lakini pia kwa kuyajua mapenzi na makusudi ya Mungu kwetu, unapojitambua maana yake utayajua makusudi na haki yako, kadharika na wajibu wako kwa ajili yako menyewe, kwa wengine na kwa Mungu pia.

Mfano pia,
WAGALATIA 3:1............... Mtume Paulo anazidi kuuonesha UTUNGU kama mama aliye karibu kujifungua mtoto kwa ajili ya kanisa la Kristo Yesu.
 Uchungu huu uliokuwa ndani ya Paulo ulikuwa ni tabia ya Mungu mwenyewe ndani yake kwa ajili ya kanisa la Kristo mwanae,
Mungu anakumbuka namnaalivyolinunua kwa gharama kubwa sana alipojitoa nmwenyewe hata kuutoa uhai wake na kuimwaga damu yake pale Kalvari kwa ajili ya wengi.

Hivyo anapoona kanisa linaenenda kinyume na mapenzi yake, Mungu anaumia sana sana na kulionea uchungu na hata kulililia.


Zaidi sana kaitabu hiki cha Wagalatia kimebeba ujumbe
SHERIA/ TORATI, NEEMA, IMANI NA HAKI.
             WAGALATIA 6:1-5........................
            Katika yote haya tunajifunza nakuona kwamba maonyo yanatakiwa yafanyike kwa ustadi mzuri sana, zaidi katika Upendo wa kweli na katika HEKIMA ya Mungu mwenyewe.

    Inapotokea miongoni mwetu FARAKA imejitokeza hatuelewani, au watu kadhaa miongoni mwetu na popote pale hawaelewani, yatupasa kusuluhisha na kuonyana kwa Upendo na Upole katika hekima yote.

===================> Lakini pia yatupasa kujifunza kumtii sana Roho Mtakatifu, kumsikiliza na kumtumiapale inapostahili kwa wakati maalumu na kwa kusudi maalumu.

KUTENDA MEMA
Galatia 6:9-"................ na tena tusichoke katika kutenda mema, maana ............................"

Kutenda mema ni changamoto kubwa sana kwa wanadamu, kwa kuwa anaona atamnufaisha mwingine pasipo yeye kupata faida.
Ndio maana wengi wanaanglia faida kwa jinsi ya mwilini wakaisahau bfaida ya rohoni.
YA JUU ZAIDI
             Ni mambo mengi sana ambayo wanafunzi wengi wamejaribu kuyaelezea kila mmoja, kweli hakika wameyaeleza mengi na hisia zao kwa namna walivyokielewa kitabu hiki na kuguswa na Ujumbe mzito uliobebwa ndani ya sura hizi zote sita za kitabu cha WAGALATIA.

               MUNGU WANGU WA MBINGUNI AZIDI KUKUINUA NA KUKUBARIKI NA AKUVUSHE KATIKA VIWANGO VINGINE VYA IMANI NA KUZIDI SANA KUMUELEWA MUNGU.

               Unapokuwa umejifunza na kuuelewa ujumbe wa Neno la Mungu unatakiwa sasa tena kuuhamishia katika maisha yako ya kimwili na ya kiroho pia.
Ndivyo maisha yako yatakavyobadilishwa na kuhuishwa na kuinuliwa juu katika viwango vingine. 

Ni mimi ndugu yako niliyekufikishia ujumbe huu Ev. Elimeleck S Ndashikiwe


Senior Pastor Boniphace Mbise
Assistant Pastor Omery Deo

                              MAHALI HAPA PANATISHA KAMA NINI!
                              HAPA NI NYUMBA YA MUNGU............ 
                                        Mwanzo 28:16-17.


PENTEKOSTE HEMA YA SIFA, TEGETA-DSM, TANZANIA.

               .......................Kariiiiibuni.............................







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

JE, UNAIJUA KARAMA YAKO? By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe