KUIKULIA IMANI

MH; EV. SAMSON JOHN
SOMO; IMANI ILIYO THABITI

              Tunapata maana za aina mbalimbali kuhusu neno hili imani, Mwandishi wa kitabu cha
Waebrania 11;1 anasema kuwa Imani ni hakika ya mambo na ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 

            IMANA ni kutegemea, kusadiki, kutazama na kutumaini. Imani yoyote ile huambatana na uaminifu na kuamini kile unachodhania kuwepo kwake au kuwa.


AINA YAIMANI
            Katika ulimwengu huu kuna aina mbalimbali za imani ambazo tunaweza kuziweka ktk makundi yafuatayo-;
[a] Imani ya asili {kibinadamu}
[b] Imani ya kiroho {kiMungu}
[c] Imani ya madhehebu 

Imani yoyote ile ina chanzo chake, na utendaji kazi wake, chanzo cha imani yoyote ni kusikia.
Hivyo inategemea umesikia nini na umesikia kwa nani.

            IMANI YA ASILI [KI-BINADAMU]
             Imani hii  chanzo chake ni kutoka kwa wanadamu wenye asili hizo.  Imani ya namna hii hufanya kazi kwa kutegemea milango mitano ya fahamu ambayo ni [KUSIKIA, KUONA, KUONJA, KUGUSA NA KUNUSA].

Tunajifunza kwa Tomaso mwanafunzi wa YESU aliyeingiwa na Imani ya namna hii. YOH 20:24

      Mtu yeyote mwenye imani ya namna hii hawezi kupokea kitu cha aina yoyote ile kutoka kwa MUNGU kama vile uponyaji, wokovu n.k [Soma 1KOR 1:18], Hivyo imani hii ni tofauti kabisa na imani ya kiroho.

           IMANI YA MADHEHEBU
Imani ya aina hii zaidi hufuata mapokeo ya kibinadamu zaidi na kuiacha kweli zilizowekwa wazi na BIBLIA.         
KOLOS 2:8, Efes 5:6-7


          IMANI YA KI-MUNGU [KIROHO]
          Imani ya aina hii zaidi inawahusu watu ambao wanaishi katika mapokeo ya MUNGU tu. Imani hii chanzo chake ni kusikia NENO la Kristo
    Rum 10;17 chanzo cha imani ni kusikia kunakotokana na Neno la Kristo.

      Hivyo basi ili mtu ampokee Yesu Kristo lazima chanzo zaidi awe amesikia chochote kumhusu huyu YESU.
Yohana 17:20, 17:8
Msingi wa imani ya ki-Mungu ni Yesu Kristo mwenyewe,
 soma Efes 2;20 na Waebr 12;1-2, Rum 21;3

Mungu wangu wa mbinguni awabariki sana na kuwalinda...............................

Somo litaendelea...........................

KARIBU SANA KATIKA IBADA ZETU ZINAZOENDELEA KANISANI

KANISA LA PENTEKOSTE HEMA YA SIFA, TEGETA KIBAONI.










Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

JE, UNAIJUA KARAMA YAKO? By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe