MOYO ULIOJERUHIKA

MH; PASTOR OMERY DEO
SOMO: THAMANI YA MOYO WAKO

              Bwana Yesu Kristo asifiwe sana mtumishi wa MUNGU na mtenda kazi shambani mwake Bwana. 
Nipende kuchukua nafasi hii kukufikishia ujumbe huu ambao Bwana amenipatia nikuletee wakati huu.

              Ni muda mrefu nimekuwa nikitafakari j\sana juu ya kitu kinachoitwa MOYO, nikajaribu kulinganisha katika
               MWA 1:26-27 Ambapo Mungu anasema ya kwamba "na tumfanye mtu kwa sura yetu na kwa mfano wetu....................."
 
       Nikapiga picha juu ya kitu kinachoitwa moyo wa mwanadamu, nikajiuliza maswali mengi sana.
Ndipo Bwana akasema nami ya kwamba MOYO ni kitu ambacho Mungu amekiumba na kukifanya kama makazi yake ndani ya mtu.

               Muda wote anapohitaji kumtembelea mwanadamu lazima afikie kwanza ndani ya moyo wake, ndipo huweza kuanza kazi yake ile aliyoikusudia kuifanya kwa mtu husika.
Akanisemesha pia  katika
                          KUMBUKUMBU  23:14 Kwa kuwa Bwana Mungu wako, yuatembea ktk kituo (MOYO) akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako, kwa hiyo na kiwe kisafi kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa nsafi, akageuka na kukuacha.

                     NB: Kumbe MOYO wa mwanadamu ndicho kituo ambacho Mungu hufikia kwanza kabisa pindi anapokuwa na ziara ya kumtembelea mtu wake.
             Hivyo basi ni lazima muda wote mioyo yetu iwe safi ili Mungu asikose mahali pasafi akaketi, kwa kuwa yeye ni msafi kuliko kitu chochote kile.

             MWANADAMU AMEAGIZWA KUULINDA MOYO WAKE 
         Mithali 4;23 Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemichemi za uzima wako.

           Marko 12;30 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote....................................

                     Unaweza ukajionea vile Mungu anataka tuwe, lakini pia anasema kuwa kazi ya moyo ni kumpenda Bwana.


UBARIKIWE SANA 
Somo Litaendelea..............................................

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

JE, UNAIJUA KARAMA YAKO? By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe