SOMO: BEBA MSALABA WAKO MPAKA MWISHO
With PASTOR OMERY DEO SHINZE
Msalaba ni alama ya UPATANISHO AU KUJUMLISHA,
Kwa sababu palikuwa na utengano ndipo Yesu Kristo akaja akautumia Msalaba ili atuunganishe, kwa maana tulikuwa tumetengwa mbali na MUNGU Baba.
Msalaba wako inatakiwa uubebe usiwaguse watu wengine maana huo unakuhusu wewe mwenyewe.
LUKA 29:23-24 Ajitwike Msalaba wake .........anifuate......
Yesu anaongea juu kuubeba Msalaba,
Msalaba huu si kitu kingine Bali ni Changamoto unazopitia.
.....Carry the cross daily.
Mara nyingi MTU anapokuwa na jaribu lolote hatakuwa tayari kupambana na hilo jaribu peke yake,
Bali hutafuta MTU mwingine aanguke naye,
NB:
USIWABEBESHE WENGINE MATATIZO YAKO.
Wana wa Israeli muda mwingi waliishia kumnung'unikia MUNGU,
Na adhabu waliyopewa wengi wao hawakuingia mji wa Kaanani.
KWENYE KUBEBA MSALABA ULIONAO JIHADHARI USICHUME DHAMBI YA PILI kwa Msalaba wako mwenyewe,
Utazichumaje?
Wengine wako makanisani kama mizani ya kupimia uzito wa mizigo.
Muda wote yupo kupima IMANI ya wengine,
Yeye hata siku moja hawazi kuhama kanisa, Bali yupo kukosoa tu wengine na kuwalaumu kila kukicha,
Anafikia hatua na kuikosoa madhabahu na kuilaumu dhidi ya Changamoto anazopitia.
Galatia 6:7 Apandacho mtu ndicho atakachovuna.
BAADA YA KUWA UMEUBEBA MSALABA HUO NA KUUFIKISHA ndipo utakapoyapata Yale yote yaliyokuwa yamekungojea (Ahadi zako),.
Wafilipi 2:5-11
Ambaye yeye alikuwa yu namna ya MUNGU, ............hakuona kule kuwa sawa na MUNGU kuwa ni kitu cha kudhikamana nacho.......
Yesu akauacha Utukufu akawa kama mwanadamu akanyenyekea hata mauti.
Tujifunze kwa Yesu Kristo,
Hakuyumbishwa na MANENO ya watu, akalisimamia tu kusudi la MUNGU.
Leo hii makanisani MTU akisingiziwa jambo anachukia wengi na anahama kanisa.....
Wengine wanaanguka kiroho, wanaiacha Imani.
HASIRA HUKAA KIFUANI MWA MPUMBAVU,
yaani anakubali kuwa mpumbavu WA wapumbavu kabisa.
NB: Jaribu ulilo nalo limekufikia kwa sababu MUNGU ameona ndio kiwango chako, Mungu hawezi kukupatia Msalaba ambao hautakuwa na uwezo wa kuubeba,
DON'T CRY AND GIVE UP.
Don't decide to pass through short cut way,
Galatia 5:...... Tunda la Roho.........
Kwa kushindwa kwako kuubeba Msalaba, unajikuta na Tunda la Roho linatoweka ndani yako.
Mbebe YESU Kristo pekee maisha ni MWAKO.
Barikiwa mno aiseeeee Mtumishi.
Maoni
Chapisha Maoni