USIIRUHUSU AMANI YA MOYO KUTOWEKA

By Ev. Elimeleck Ndashikiwe

        Watu wengi wamekuwa wakikaa na majeraha ya maumivu ya moyo kwa muda mrefu bila ya kuyatafutia matibabu.

      Matokeo yake majeraha hayo yanazidisha maumivu ndani ya mioyo yao na wakati mwingine kupelekea kuwatoa kabisa kwenye mpango wa Mungu.

        Njia ya kwanza na ya muhimu kuponya majeraha ya moyo ni kulizungumzia jambo lililosababisha wewe kupata maumivu ya moyo.

Unapoongea na mtu juu ya jambo hilo itakusaidia kukupunguzia maumivu ya moyo. Kuongea huku kutakusaidia kuikubali hali halisi na kuendelea mbele na maisha yako.

         Kama binti aliyeokoka na kumjua Mungu, mtu wa kwanza kumwambia jambo hilo ni Bwana Yesu.

         Zaburi 34:18
  BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo na huwaokoa waliopondeka roho.

Mweleze Mungu jinsi unavyojisikia, jinsi moyo ulivyoumia na uongee naye kama rafiki aliye karibu mwenye uwezo wa kukusaidia.
         Unapomwambia Mungu jambo hili utaona AMANI yake inaingia ndani ya moyo wako na kuyaondoa maumivu yote uliyonayo.

            Pia uwe karibu na marafiki zako ambao wanamjua Mungu na ambao wako tayari kukutia moyo na kukufariji. Kisha samehe kabisa na kusahau.

        Kuna nguvu kubwa ya kuponya maumivu ya moyo katika kusamehe. Halafu uyajali maisha yako na weka nguvu zako katika mambo ambayo yanakufanya ujisikie unafaa na unathamani.

         Endelea kumtumikia Mungu kwa bidii, fanya kazi zako kwa juhudi na maarifa na ujali na uupende mwili wako.

JIONE KUWA WEWE U WA THAMANI, NA BILA WEWE DUNIA ITAHARIBIKA.
Mbingu inakutegemea, Nchi nayo inajivunia wewe ktk ustawi.

   2 Nyakati 7:14-15
.........Mungu anaiponya nchi kupitia wewe

Ubarikiwe na Mungu wa mbinguni.

Ni Mimi ndugu yako mwalimu na mwinjilisti
ELIMELECK NDASHIKIWE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

NGUVU YA HASIRA