MUNGU ANAKUWAZIA YALIYO MEMA NYAKATI ZAKO ZOTE

NINI KIKUTENGE NA UPENDO WA MUNGU?


Ndiyo! Ziko changamoto nyingi Sana za maisha zaweza kukifanya uyumbe au upoteze Ile nguvu ya asili kukifanya usonge mbele, 

Hakuna kitu KIKUBWA Kama kumtegemea Mungu, na kuendelea kuzitunza Ile asili yako ya kiMungu ndani yako.

Watumishi wa Mungu tukiwa pamoja katika moja ya siku baada ya kutoka ibadani (Jerry Okatch, Joseph Okaka na Elimeleck Ndashikiwe)!


      Kwenye Maisha Hakuna Kitu kibaya Kama Kurudi nyuma na Kuacha Kupiga Hatua njema ulizokuwa unapiga 

     Na Haijalishi Unayopitia, Haijalishi Hali uliyonayo, Haijalishi Mazingira magumu unayopitia Lakini Kamwe *YASISABABISHE WEWE URUDI NYUMA* 


      `Yasisababishe Wewe urudi nyuma Kwenye ibada, urudi nyuma Kwenye Maombi, urudi nyuma Kiroho,urudi nyuma Kwenye bidii na Juhudi uliyokuwa nayo Kwa MUNGU'


 Ndiyo Maana Maandiko Yanatuambia👇👇

 Mithali 1:32
      Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua,  Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.

HAKIKISHA WAKATI WOTE KWENYE MAISHA YAKO PIGA VITA KURUDI NYUMA NA USIKUBALI KAMWE KURUDISHWA NYUMA NA KITU CHOCHOTE

HAIJALISHI AWE NI MTU ,YAWE NI MAZINGIRA, IWE NI HALI YOYOTE, IWE CHANGAMOTO YOYOTE ILE ISIKUFANYE URUDI NYUMA KATIKA MUNGU

Wewe endelea tu kumtumikia Mungu kwa uaminifu na Moyo wa kupenda bila kubembelezwa, utauona Uzuri wa Mungu katika maisha yako.

Yeremia 33:2
     2 Bwana alitendaye jambo hili, Bwana aliumbaye ili alithibitishe; Bwana ndilo jina lake; asema hivi,

3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

22 Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi wanaonihudumia.


 ```BALI HAKIKISHA KILA WAKATI UNAKUWA MTU WA KUSONGA MBELE NA UWE WA KUPIGA HATUA ZAIDI KWENDA MBELE``` 

 NEEMA YA BWANA YESU IWE PAMOJA NAWE

Mwana PENTEKOSTE HEMA YA SIFA

By www.hemayasifachurch.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KIROHO

WATUMISHI WA MUNGU TUSIDHARAULIANE

JE, UNAIJUA KARAMA YAKO? By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe