Machapisho

ROHO MTAKATIFU

“ROHO MTAKATIFU ANAWEZA KUHUISHA MAMBO YALIYOKUFA;  -Maandiko yanena YEYE ALIYEMFUFUA YESU ATAIHUISHA NA MIILI YENU ILIYO KATIKA HALI YA KUFA!. -Katika MAONO ya EZEKIELI, YALE MAJI YA MTO YANAWEZA KUHUISHA KILA KILICHOKUFA, HATA YALIPOFIKA KWENYE BAHARI (BAHARI MFU) MAJI YAKE YALIPONYEKA;  •BILA KUJALI MAISHA YAKO YAMEKUFA, BILA KUJALI MAMBO YAMEKUFA NA HAUNA MATOKEO YOYOTE; ROHO WA MUNGU ANAWEZA KUYAHUISHA TENA YAKAWA HAI!.  •IKIWA UMEINGIA MWEZI MPYA, MWEZI WA NNE; MRUHUSU ROHO WA MUNGU AYAFUFUE MAMBO YAKO YALIYOKUFA. IKIWA ROHO YAKE ALIYEMFUFUA YESU ANAKAA NDANI YAKO, YEYE ANAWEZA KUYAFUFUA MAMBO YAKO..       MWEZI HUU MPE NAFASI YA KUTOSHA, KILA KILICHOKUFA KINAWEZA KUWA HAI TENA MRUHUSU ROHO WA YESU AHUISHE!!.  “Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale yataponyeka, na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia...

HAKUNA CHOCHOTE KATIKA  MAISHA  CHA KUPIGANIA! 

Picha
UKWELI MCHUNGU,  MWANADAMU ACHA KIBURI NA MAJIVUNO By Ev. Elimeleck Ndashikiwe  Nguo zako zile bora kabisa kuna mtu kwake ni matambara tu.  Akiba yako kwenye akaunti ya Benki ni sawa na mchango wa mtu katika sherehe tu.         Boyfriend au Girlfriend wako au mchumba ni Ex wa mtu! Hivyo ni nini hasa cha kujivunia? Maisha ni mafupi sana na madogo mno kujisikia kuwa mkubwa ama bora kuliko mtu wengine.        "Tupo sote uchi hadi kufa" aliwahi kusema Steve Jobs. Gwiji muanzilishi wa iPhone(ambaye kwa sasa kifo kimemchukua kwa maradhi ya Cancer) "Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa sote Kukabiliwa na kifo".  Mhubiri 3 1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote. 15 Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.     ...

KITABU CHA YOHANA MTAKATIFU

Picha
Bwana Yesu asifiwe sana wapendwa, Mistari muhimu: "Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu ... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli "(Yohana 1: 1,14). "Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, 'Tazama mwana kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:29). Ev. Elimeleck Ndashikiwe   "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe Pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16). "Yesu akajibu, akawaambia, 'Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwaamini yeye aliyetumwa na yeye" (Yohana 6:29). "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu. Mimi nilikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yohana 10:10). "Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu" (Yohana 10:28). ...

HEMA YA SIFA KISANGA B

Picha
Huu ni mwaka ambao tumeanza kwa ushindi mno mno, Mungu ametuwezesha zaidi ya fahamu zetu na akili zetu! IT IS A NEW BEGINNING IN 2024 Matukio katika picha mojawapo ya ibada zetu kanisani. Our Bishop BONPHACE MBISE

MUNGU ANAKUWAZIA YALIYO MEMA NYAKATI ZAKO ZOTE

Picha
NINI KIKUTENGE NA UPENDO WA MUNGU? Ndiyo! Ziko changamoto nyingi Sana za maisha zaweza kukifanya uyumbe au upoteze Ile nguvu ya asili kukifanya usonge mbele,  Hakuna kitu KIKUBWA Kama kumtegemea Mungu, na kuendelea kuzitunza Ile asili yako ya kiMungu ndani yako. Watumishi wa Mungu tukiwa pamoja katika moja ya siku baada ya kutoka ibadani (Jerry Okatch, Joseph Okaka na Elimeleck Ndashikiwe)!       Kwenye Maisha Hakuna Kitu kibaya Kama Kurudi nyuma na Kuacha Kupiga Hatua njema ulizokuwa unapiga       Na Haijalishi Unayopitia, Haijalishi Hali uliyonayo, Haijalishi Mazingira magumu unayopitia Lakini Kamwe *YASISABABISHE WEWE URUDI NYUMA*        `Yasisababishe Wewe urudi nyuma Kwenye ibada, urudi nyuma Kwenye Maombi, urudi nyuma Kiroho,urudi nyuma Kwenye bidii na Juhudi uliyokuwa nayo Kwa MUNGU'  Ndiyo Maana Maandiko Yanatuambia👇👇   Mithali 1:32       Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua,...

KIJANA NA UTAKATIFU KATIKA KRISTO YESU

INJILI YA AMANI UTANGULIZI:        Nakukaribisha msomaji katika tafakari ya somo jingine linalohusu kijana na maisha ya kikristo ni jinsi gani kijana aishi maisha Matakatifu kama inavyompendeza Mungu na si kuwafurahisha tu wanadamu katika maisha yetu tukimchukiza MUNGU.     Kristo ni mpakwa mafuta. Ambaye ni tofauti na watu wengine. Sasa basi Ukiwa kama kijana wa kikristo ambaye umebatizwa kwa Roho Mtakatifu ndani mwako na si tu kwa ishara ya Wanadamu ya nje tambua kuwa Mungu amekuweka kwa kusudi lake kama mpakwa mafuta umzalie matunda kwa njia ya Kristo YESU.      WARUMI 7:4         “Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda”.      Hivyo basi ili kijana wa Kijana wa ki...

UTUKUFU KWA JEHOVAH

Picha
INJILI iliyohubiriwa Dodoma Chamwino haikuwa ya kitoto kabisa, Mungu wetu alituwezesha kuwafikia wengi, na wengi walifunguliwa na kumpokea Yesu Kristo na kumfanya kuwa Bawana na Mwokozi wa maisha yao. Namaanisha WALIOKOKA. Kwaya ya PHS-Choir ilihudumu mkutanoni hapo na kuwabariki wengi kwa utukufu wa jina la Yesu Kristo.