ANAYESTAHILI KUABUDU NI YUPI?
MH: EV. SAMSON JOHN SOMO: KUABUDU Kuabudu maana yake ni kitendo cha kumkaribia MUNGU au chochote kile kwa kukitukuza katika madhabahu ya aina yoyoyte ile. Kwa maana nyingine twaweza kusema kuwa,kuabudu ni kufanya tendo la kifalme ktk madhabahu na kutoa dhabihu kimiungu. ISAY 43:7 `Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemuumba kwa ajili ya utukufu wangu., mimi nimemumba, naam, mimi mnimemfanya. Hapa tunaona namna ambavyo MUNGU mwenyewe anajitambulisha kwa watu wote kuwa yeye ndiye alliyewafanya na kuwaumba. Hivyo basi, kwa sababu hiyo, Kila yeyote aliyeumbwa na kufanywa na MUNGU, anatakiwa kujua ni wapi anastahili kuelekeza ibada yake. ...